#peopleareawesome, Gumzo Mitaani

MKIRITIMBA

Asema Sahibu:

Mkiritimba mmoja kasimama mbele ya vijana kijijini ndoo ikiwa mbele yake na huku kando akiwa amewekelea mawe makubwa, changarawe, mchanga na maji.

Basi akawauliza wale vijana, “Je, mwaamini ya kuwa naweza jaza ndoo hii na vitu hivi vyote?”

“La hasha…havitatoshea bwana…” walijibu vijana wa kijiji.

Wakati huo, mkusanyiko ulikuwa wazidi kufura…

Wengi walimjua huyu mkiritimba wakitaka kuuona ujinga wake peupe.

Basi, jamaa huyu akachukua yale mawe makubwa akayamwaya ndani ya ndoo yake…

“Je, ndoo ishajaa?” akauliza…

“Ndio. Haitatoshea chochote zaidi bwana wee…” wakalia vijana.

Ah, mkiritimba akachukua mfuko wa changarawe akamwaya chembe chembe zote ndani ya ile ile ndoo…

Halafu akaitikisa ile ndoo ili changarawe ziingie katikati ya mawe makubwa.

“Je, ndoo ishajaa?” akauliza tena…

Vijana wakaangaliana kwanza halafu wakasema, “Ishajaa bwana wee…”

Mkiritimba akauchukua mchanga akaumwaya ndani ya ile ile ndoo halafu akaitingisa kikamilifu.

Wakti huo, vijana walikaa kama wameduaa…

Mkiritimba hakuwauliza chochote zaidi.

Badala yake, aliichukua chupa ya maji akayamwaya ndani ya ile ndoo.

Doo! Maji yaliingia ndani na hayakumwaika nje!

Mkiritimba akawatazama vijana akawauliza, “Mwataka kujua funzo?”…

“Ndio…” vijana wakajibu.

“Mawe makubwa ni mambo muhimu zaidi maishani…jamii, furaha, marafiki… Hakikisha unayaweka kwanza katika maisha yako”

“Zile changarawe ni mambo yanayo na umuhimu fulani maishani lakini hata yakipotea, bado utajisimamisha usonge mbele…kazi, biashara…”

“Na yale maji je?” wakauliza vijana…

“Yale maji!” Mkiritimba akaendelea, “Yale maji ni pesa…”.

“Pesa zaja halafu zapotea. Ukiziweka juu zaidi ya yote, utasononeka…utapoteza mengine yote kwani kama ningeanza na maji, basi yale mawe hayangetoshea”.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s