#peopleareawesome, Gumzo Mitaani

‘MOSHI WA MANYASI’

Asema Sahibu:

Walikuwa jamaa wawili ambao watu wa Nairobi watawaita ‘wasee’…

Hawa jamaa walikuwa wamevuta ‘moshi wa manyasi’ fulani wakitia stori maskani…

Walipohisi kuboeka, wakanong’onezeana kurudi zao mtaani…

Lakini njia ya mtaani haikuwa tambarare…

Wakitembea walikuwa wausikia ‘moshi wa manyasi’ ukiwanong’onezea akilini…

Wakaingia mori na jadhba…

Wakatia bidii wakitembea kwa mbio…

“Jamaa tuharakishe au tutachelewa”, mmoja alimwambia mwingine…

“Eeh! Nasikia kaa kupeperuka mimi!” akajibu yule mwingine…

Kidogo kidogo wakafika kwa kichochoro…

Barabara ikawa nyembamba zaidi wasiweze kutembea kwa pamoja…

Mmoja wao akasikia ‘moshi wa manyasi’ ukimpatia maarifa akilini mwake:

“Hebu tuusukume ukute upanuke ndio tutembee pamoja sweba…”

Jamaa wakaanza kuusukuma ukuta wa nyumba ili barabara ipanuke…

Wakausukuma…wakausukuma…wakausukuma…

Jasho likawatoka mpaka wakaamua kuyavua mashati na kuyaweka chini…

Wakendelea kuusukuma ukuta…wakausukuma…wakausukuma…wakausukuma…wakausukuma…

Jamaa fulani aitwaye ‘dingoo’ alikuwa yuawatazama kwa umbali…

Alipoona wameshasahau shati zao, akajinyakulia bidhaa…

Huyo katoweka asipatikane…

Kidogo kidogo jamaa zetu walipogeuka wakaona…ala! hamna mashati…

“Eeh Sweba! Shati hamna!….”, mmoja akamwuliza mwenziwe…

Mwenzake naye akaanza kuangua kicheko cha kimataifa…

Akacheka…na akacheka…na akacheka…na akacheka…na akacheka…

“Wacheka nini sweba?” akaulizwa na mwenzake…

“Sweba! Sikudhania tutausukuma ukuta huu…angalia vile tumeusukuma kwa umbali mno hadi hatuoni shati zetu…hehehehe”.

Ndugu wee…Tahadhari na ‘Moshi wa Manyasi’…

Asema Sahibu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s