#peopleareawesome, Gumzo Mitaani

HATIA YA U’HASLA’

Hii ni risto ya bazenga anaitwa ‘hasla’.

Manzee lyfe imemkulia vako design moja mbaya sana.

Na huyu si hustler yule wanasiasa wanadai…

Hajamdhulumu yeyote…

Hajamperemba msee yeyote…

Hajaleta risto za ovyo na kuenjoy wasee na uwongo…

Huyu ni msee amekulia rough jo!

Tangu kuzaliwa kwake, amejua kuwa lyfe haina huruma hata kama mtaa wake unaitwa Huruma…

Githomo kilikatika mapema juu mapero walikuwa hawana doo…

Ikabidi atafute mbinu zingine sa kujitafutia…

Mapero walikuwa ‘missin in action’ na instead akaanza kazi ya upero kwa mabro na masis wake wasmall…

Kuhasl haikuwa rahisi…

Umakanga hapa…

Kushainisha ndula pale…

Kuuza scrap metal hapa…

Kufungua obando ya kudema pale…

Hata biarasha duu alitry…

Kuuza tei ya kichakani hapa…

Kufanya magendo pale.

Hakuwa na otherwise…

Ilibidi kutafuta mbinu ya ku-survive kwa vile kulikuwa na midomo inamgojea kwa keja…

Alitry asijihusishe na mbogi za kusafisha…

Alitry asiingie kwa risto za kuchapia wasee…

Alitry asiwe dingo hata kama alikuwa msoto deadly…

Imani yake haikumruhusu…

Alitia bidii kwa ile janta ilikuwa mbele yake ndio asongee…

Lakini still lyfe ya ghetto ilikuwa imemkalia ngumu…

Mara kwa mara mbogi za kusafisha zikiwatape wasee walami,
masansee walikuwa wanaachiliwa mtaani kuhangaisha wasee…

Hata mmoja wa beste wake wa nguvu alikuwa amewahiwa na ndeng’a usiku mmoja akitoka wera…

Na si yeye pekee…

Kuna wengine ambao walikuwa wamelazwa na bunde za masansee mwitu…

Walikuwa wakienda ukumbusho kila mwaka pale Lang’ata…

Na lyfe ilizidi kuwa vizii zaidi haswa wakati wa curfew…

Ilibidi kufunga wera mathenashara…

Alikuwa akisikia walami wakibonga kingosoo mingi juu ya ‘social distancing’, ‘wearing masks’, ‘washing hands’ na kadhalika…

Kitu ilimshinda ni angepata maji ya kuosha mkono wapi wakati hata hawakuwa na maji ya kunywa kwa keja…

Wangeji ‘social distance’ kiaje na walikuwa wanaishi wasee kindee kwa keja yao small…

Wangelipia aje keja na janta ilikuwa imekatika kwa sababu gethaa ya curfew ilikuwa inakatsia…

Wangedema nini na doo zilikuwa less kuruka!…

Risto hii yote ya Corona ilikuwa inadai lyfestyle ambayo hawange’wesmake’…

Isitoshe, jioni jioni hivi, masansee mwitu walikuwa wanatokelezea kighafla kuharass wasee wanyonge…

Hata jirani yake bado ako hosi baada ya kupigwa vibaya…

Saa hii wanaendelea kumchangia niado za kumtoa hosi…

Lakini vile situation ni gwan, so far wame-collect rwabe tu na watoi wake wanaumia…

Huyu msae alikuwa hawker pale stage ya bu na alikuwa anahepa ajusinde kejani kabla ya kupatana na masansee…

Bahati mbaya, alichelewa na dakika mbau akavamiwa kwa marungu…

Walijaribu kumsifia kesi yake kwa wasee wa Human Rights lakini hadi saa hii wako ‘waiting mode’…

Na hii kesi sio ya kipekee…

Wasee hawana hatia wamekuwa wakiuliwa na masansee mwitu kila siku…

Lakini wasee wa mtaani wakizusha hawasikizwi…

Wanaonekana ni kama ni wasee wa fujo tu…

Wanaambiwa wacheze chini…

Kesi yao itaamuliwa…

Na si risto ya police brutality pekee…

Mabazenga kibao mtaani hawana wera…

Na sio kupenda kwao…

Wengi wao wana githomo lakini janta zina wenyewe…

Wale wanajuana kwa maofisi.

Lyfe ya u’hasla’ sio lyfe ya ‘hustler’…

Hasla ni sweba wa mtaani anakula rough daily…

Hustler ni polytrickcian anaye-tukulia vako eti yeye anatuelewa lakini cha ukweli anadema manono…

Hasla ni msae anaye-struggle na bizna yake ndogo ili aweke dema kwa meza…

Hustler ni polytrickcian anayetubeba ufala sana;

Msee hajatoa jasho kujenga bizna yoyote…

Yeye ni kujaza mifuko kupitia ukauzi wa umma…

Hasla ni ule msee masansee mwitu wanamchangamkia ili kutoa frustrations zao…

Hustler ni polytrickcian anayelindwa na hao masansee…so watamchangamkia aje?

Hasla anajua hakuna otherwise…lazima afanye vile anaweza aeke dishi kwa meza…iwe ni kuuza makaa au kuwa makanga au ku-push benta…kama mbaya mbaya…

Hustler ni polytrickcian ako na mabeshte masonko watakaomchangia akiingia kwa risto noma…

Lyfe ya hasla sio lyfe ya hustler.

Natumai kama Wakenya tutatia akili tunapowachagua ma-polytrickcian next time.

Au sio…

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s